UJUE MJI WETU WA UJIJI
Ujiji ni mji upande
wa Magharibi wa Tanzania
mwambaoni kwa Ziwa Tanganyika. Ni mahali pa kihistoria na mji
wa kale katika magharibi ya Tanzania. Iko kilometa 10 tu upande wa Kusini wa
mji wa Kigoma.
Ujiji huaminiwa
imeundwa mwanzoni mwa karne ya 19 labda kidogo baada ya mwaka 1821 [(makala
"Udjidji" katika DKL]. Ilikuwa mwisho wa njia ya misafara kati ya
pwani la Bahari Hindi na Ziwa Tanganyika. Bidhaa kutoka
pwani zilihifadhiwa hapa katika ghala na kusambazwa kwa biashara ya kuvukia
ziwa kwa mashua. [[ Wapelelezi]] Wazungu walianza kufika wakati wa Tippu Tip.
Ni mahali ambapo Richard Burton na John Hanning Speke
walifikia Ziwa Tanganyika mwaka wa 1858, na tena ambapo Henry Morton Stanley alimkuta David
Livingstone mwaka wa 1871.
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani
umuhimu wa Ujiji ulipungua. Mwambao ulifaa mashua ya kienyeji lakini kina
hakikutosha kwa ajili ya meli mpya. Hivyo makao makuu ya utawala yalipelekwa
Kigoma penye bandari nzuri.

No comments:
Post a Comment